Dominika ya 5 ya Kwaresima
· Mwaka C · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Isa 43:16-21atoaye gari na farasi, jeshi la askari na uwezo; wamelala, hawataondoka; wametoweka, wamezimwa mfano wa utambi. Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani. Wanyama wa kondeni wataniheshimu, mbweha pia na mbuni; kwa sababu nimewapa maji jangwani, na mito nyikani, ili kuwanywesha watu wangu, wateule wangu; watu wale niliojiumbia nafsi yangu, ili wazitangaze sifa zangu.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 126Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi
Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni,
Tulikuwa kama waotao ndoto.
Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko,
Na ulimi wetu kelele za furaha.
K. Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi
Ndipo waliposema katika mataifa,
Bwana amewatendea mambo makuu.
Bwana alitutendea mambo makuu,
Tulikuwa tukifurahi.
K. Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi
Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa,
Kama vijito vya Kusini.
Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.
K. Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi
Ingawa mtu anakwenda zake akilia,
Azichukuapo mbegu za kupanda.
Hakika atarudi kwa kelele za furaha,
Aichukuapo miganda yake.
K. Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi
Somo la Pili
Flp 3:8-14Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Yoe 2:12, 13Injili
Yn 8:1-11Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
Dastani Agapitho · 6 Aprili 2025
Amina