Ijumaa. 02 Mei. 2025

Tafakari

Jumapili, Aprili 06, 2025

Jumapili, Aprili 6, 2025,

Juma la 5 la Kwaresima


Isa: 43: 16-21;
Zab 126: 3
Flp:3:8-14
Yn 8: 1-11


TAZAMA NINATENDA TENDO JIPYA


Katika somo Ia kwanza kwa njia ya nabii Isaya, tunamsikia Mungu Mwenyewe akituambia hivi: “Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama ninatenda tendo jipya.

Katika somo la pili Paulo akiwaandikia Wafilipi, anasema hivi juu yake mwe nyewe: “Nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachukulia yaliyo mbele, nakaza mwendo.”

Na katika injili, tunamkuta akinamama mmoja aliyesukumwa mbele ya Yesu. “Amefumaniwa alipokuwa akizini. Mwanaume yeye ametoweka lakini mwana mke huyo amekamatwa. Mafarisayo wamemleta mbeie yaYesu. Macho yao yana mhukumu sawasawa na maneno yao. Ha Yesu hamwangalii hata. Asiwe anamw aibisha, Yesu anatazama chini naye anawazungumzia kwanza wenye kumshtaki. Kitambo tu nao wameondoka kwa sababu wanaona kwamba hata wao wenyewe wangeweza kushtakiwa.

Yesu alifanya nini kwa ajili ya mwanamke huyo. Je, alisema kwamba alilo tenda si jambo baya? Je, alisema kwamba kwa vyo vyote si vibaya sana kulala na mtu asiye mumewe? Hata. Ha alimsaidia aende mbele. Asahau mambo ya zamani na kutazama siku za usoni

“Hakuna aliyekuhumu kuwa na hatia?
Wala mimi sikuhukumu.
Enenda zako; wala usitende dhambi tena.”

Yesu anasahau na kusamehe mambo yake ya zamani. Ndivyo Munçu alivyo Ndivyo alivyokuwa amefanya kwa ajili ya Taifa lake —taifa Ia Israeli - kabla ya Yesu kuja ulimwenguni petu. Mungu anawaita: “Wateule wangu”. Hata ikiwa taifa lake wamekuwa wanamkosea uaminifu mara nyingi sana. Hata ikiwa mara nyingi mno wamekwenda mbali naye wala hawakutii amri zake, Mungu anawaambia waya sahau mambo ya zamani na kuona “tendojipya”analowafanyia. Anawasamehe tena na kuwaokoa.

Ndivyo Mungu wetu alivyo: Mungu anayeangalia mambo yetu ya zamani ili kuyasamehe ikiwatunayasikitikia hayo tuliyotenda. Ndiye Mungu mwenye kuele keza macho na mioyo yetu kwa siku za usoni. kwa hayo anayotuandalia Yeye

Ndio hasa ujumbe wa injili - Habari Njema ambayo sote twahitaji kuisikia. Mungu hataki kutuona tunasukuma makosa yetu ya zamani na kushindwa kwetu kama mzigo mzito. Mungu haoni furaha kutuona tunatembea tukiwa na nyuso zenye huzuni na mioyo mizito kwa ajili ya mzigo wa dhambi zetu za zamani.

Wapo watu wengi walio kama Bernardo. Labda ndiyo mapatano ya kibia shara yalioshindikana na mtu amepoteza akiba ya pesa ya maisha yake yote. Kwa kijana, yawezekana kwamba ameshindwa mtihani ambao ungalimfungulia m lango wa kazi mpya. Labda ndiyo magombano kati ya ndugu wafamNia moja. Wameam biana maneno makali, mmojawao ametoroka bila kurudi hata. Yawezekana kuwa mtu fulani amemwua mtoto kwa gari lake. Kumbukumbu hilo lazidi kukaa na mtu huyo Usirnwachie raha hata kidogo.

Watu hawa wamekwama katika mambo yao ya zamani. Nina hakika kwamba umewahi kuona, wakati wa masika, jinsi gari kubwa Ia mizigo liwezavyo kuzama matopeni. Dreva aweza kujaribu sana kulitoa kutoka katika matope, lakini gari Ii nazama zaidi. Ndivyo waUvyo watu wengine: wao wajitahidi kujiweka huru wenyewe kutoka kwa mambo waliyoyasema na kuyafanya zamani, lakini wanashindwa.

Makumbukumbu mabaya, masikitiko, na hall mbaya mno ya kujisikia kuwa hawawezi kuyafuta kabisa mambo ya zamani. Mambo hayo yote yawalemeza watu. Wanajisikia wamepondwa na mzigo wa namna hii. Wangependa kuwekwa huru kutoka kwa mzigo huo, ila upo nao siku zote, mchana na usiku.

Lakini yupo Mmoja awezaye kutuweka huru kutoka kwa mziço wetu Mzigo wa dhambi na hatia. Mzigo wa makumbukumbu mabaya na masikitiko. Mungu ndiye atakaye kufanya hivi. Mwanaye Yesu amekuja kwetu kwa kusudi hilo hasa. Anangoja tu tuwe tunamgeukia. Pengine, hata ndiye Mwenyewe anayetugeukia akituomba tuukubali msaada wake.

Kama ilivyomtokea mwanamke yule aliyegunduliwa katika kuzini. Aliachwa na mpenzi wake. Sasa wenye kumshtaki wameondoka naye yupo peke yake mbele ya Yesu akiogopa Yesu alimsamehe mwanamke naye alimwachia Yesu mambo yake ya zamani

Sisi vile vile mara nyingi twajisikia tumeachwa tu peke yetu na kuogopa Lakini sisi pia twaweza kusamehewa. Na tukiwa tumesamehewa, Mungu anatu omba tumwachie mambo yetu ya zamani. Lililo Ia maana hasa siyo hayo tuli yosema na kutenda. Lililo a maana ndiyo afanyayo Mungu na hayo atakayotuwe zesha kufanya na sisi wakati ujao

Tukimruhusu Mungu ayashughulikie mambo yetu ya zamani, hapotutajisikia kama Wayahudi. Katika Zaburi ya leo, tumewasikia wakisema: “Bwana alipoture jeza, tulikuwa kama waotao ndoto. Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko.” Jambo tile tile laweza kututokea sisi, ikiwa tutamruhusu Mungu atufanye tuwe wapya kwa msamaha wake.

Maisha mapya - Juma hililija uchukue muda na uone jambo gani maishani mwako ni zito kubebwa. Ujiulize kwa nini unasukuma mzigo huo. Halafu, umgeukie Bwana na umwachie jambo lo lote lenye kukulemeza tangu zamani.

Maoni


Ingia utoe maoni