Kumbukumbu ya Mtakatifu Alfonsi Maria wa Liguori
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Kut 33:7-11; 34:5-9,28Naye Bwana akasema na Musa uso kwa uso. kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha akageuka akarejea hata maragoni; bali mtumish wake Yoshua, mwana wa Nuni, naye ni kijana hakutoka mle hemani.
Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimam; pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu. Mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne. Musa akafanya haraka, akainamisha kichwa chake hata nchi, akasujudu. Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu, maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako. Naye alikuwa pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano. hizo amri kumi.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 103 : 6-13Bwana amejaa huruma na neema.
Bwana ndiye afanyaye mambo ya haki,
na hukumu kwa wote wanaoonewa.
Alimjulisha Musa njia yake,
wana wa Israeli matendo yake.
K. Bwana amejaa huruma na neema.
Bwana amejaa huruma na neema,
haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.
Yeye hatateta sikuzote,
wala hatashika hasira yake milele.
K. Bwana amejaa huruma na neema.
Hakututenda sawasawa na hatia zetu,
wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.
Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi,
kadiri ileile rehema zake ni kuu kwa wamchao.
K. Bwana amejaa huruma na neema.
Shangilio la Injili
2Tim 1:10Mwokozi wetu Yesu Kristu alibatili mauti,
na kuufunua uzima na kutokuharibika kwa Injili.
Aleluya.
Injili
Mt 13:36-43Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni