Kumbukumbu ya Mtakatifu Inyasi wa Loyola
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Kut 32 :15-24,30-34Na Yoshua aliposikia kelele za watu walipokuwa wakipiga kelele, akamwambia Musa, Kuna kelele ya vita maragoni. Akasema, Hiyo si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushinda vitani, wala si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushindwa; bali kelele za watu waimbao ndizo ninazozisikia mimi.
Hata alipoyakaribia marago akaiona ila ndama, na ile michezo. Hasira ya Musa ikawaka, akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima. Akaitwaa ile ndama walioifanya, akaichoma moto, akaisaga hata ikawa mavumbi, akainyunyiza juu ya maji, akawanywesha wana wa Israeli. Musa akamwambia Haruni; Watu hawa wamekufanyani hata ukaleta dhambi hii kuu juu yao? Haruni akasema, Hasira ya bwana wangu isiwake; wewe unawajua vvatu hawa, ya kuwa wamejielekeza kwa mabaya. Maana waliniambia, Katufanyie miungu, itakayokwenda mbele yetu, kwa maana mtu huyo Musa, aliyetutoa katika nchi ya Misri, hatujui yaliyompata. Nikawaambia, Mtu yeyote aliye na dhahabu na aivunje; basi wakanipa, nami nikaitupa ndani ya moto, akatoka ndama huyu.
Basi asubuhi yake Musa akawaambia watu, Mmetenda dhambi kuu; na sasa nitakwenda juu kwa Bwana, labda nitafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu. Musa akarejea kwa Bwana, akasema, Aa! watu hawa wametenda dhambi kuu, wamejifanyia miungu ya dhahabu. Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao - na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichokiandika. Bwana akamwambia Musa, Mtu yeyote aliyenitenda dhambi, ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu. Basi sasa uende ukawaongoze watu hawa mpaka mahali pale ambapo nimekuambia habari zake; tazama, malaika wangu atakutangulia; pamoja na hayo siku nitakavowajilia nitawapatiliza kwa ajili ya dhambi yao.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 106:19-23Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema.
Walifanya ndama huko Horebu,
Wakaisujudia sanamu ya kuyeyuka.
Wakaubadili utukufu wao
Kuwa mfano wa ng’ombe mla majani.
K. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema.
Wakamsahau Mungu, mwokozi wao,
Aliyetenda makuu katika Misri.
Matendo ya ajabu katika nchi ya Hamu,
Mambo ya kutisha penye bahari ya Shamu.
K. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema.
Akasema ya kuwa atawaangamiza,
Kama Musa, mteule wakw, asingalisimama,
Mbele zake kama mahali paiipobomoka,
Ili aigeuze hasira yake asije akawaharibu.
K. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema.
Shangilio la Injili
Efe 1 :17, 18Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo,
awape roho ya hekima mjue
tumaini la mwito wake.
Aleluya.
Injili
Mt 13:31-35Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni