Jumatatu ya 13 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Amo 2:6–10, 13–16Tazameni, nitawalemea ninyi, kama gari lilemeavyo lililojaa miganda. Naye apigaye mbio atapotewa na kimbilio; Wala aliye hodari hataongeza nguvu zake; Wala shujaa hatajiokoa nafsi yake; Wala apindaye upinde hatasimama; Wala aliye mwepesi wa miguu hataokoka; Wala apandaye farasi hatajiokoa nafsi yake; Naye mwenye moyo mkuu miongoni mwa mashujaa atakimbia uchi siku ile, asema Bwana.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 50:16–23Yafahamuni hayo, ninyi mnaomsahau Mungu.
Mtu asiye haki, Mungu amwambia,
Una nini wewe kuitangaza sheria yangu,
Na kuliweka agano langu kinywani mwako?
Maana wewe umechukia maonyo,
Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.
K. Yafahamuni hayo, ninyi mnaomsahau Mungu.
Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye,
Ukashirikiana na wazinzi.
Umekiachia kinywa chako kinene mabaya,
Na ulimi wako watunga hila.
K. Yafahamuni hayo, ninyi mnaomsahau Mungu.
Umekaa na kumsengenya ndugu yako,
Na mwana wa mama yako umemsingizia.
Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza;
Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe.
Walakini nitakukemea;
Nitayapanga hayo mbele ya macho yako.
K. Yafahamuni hayo, ninyi mnaomsahau Mungu.
Yafahamu hayo,
Ninyi mnaomsahau Mungu.
Nisije nikawararueni,
Asipatikane mwenye kuwaponya.
Atoaye dhabihu za kushukuru,
Ndiye anayenitukuza.
Naye autengenezaye mwenendo wake,
Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.
K. Yafahamuni hayo, ninyi mnaomsahau Mungu.
Shangilio la Injili
Yn 14:5Bwana anasema: mimi ndimi njia, na ukweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Aleluya.
Injili
Mt 8:18–22Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni