Alhamisi ya 31 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Flp 3:3–8Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 105:2–7Ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.
Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi,
Zitafakarini ajabu zake zote.
Jisifuni kwa jina lake takatifu,
Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.
K. Ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.
Mtakeni Bwana na nguvu zake,
Utafuteni uso wake sikuzote.
Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya,
Miujiza yake na hukumu za kinywa chake.
K. Ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.
Enyi wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake,
Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
Yeye Bwana, ndiye Mungu wetu,
Duniani mwote mna hukumu zake.
K. Ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.
Shangilio la Injili
Yn 10:27Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.
Injili
Lk 15:1-10Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione? Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea. Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni