JUMATATU YA 8 YA MWAKA
· Mwaka C
Somo la Kwanza
1 Pet. 1 : 3-9Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 111 :1-2, 5-6, 9-10Atalikumbuka agano lake milele.
Aleluya,
Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote,
Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
Matendo ya Bwana ni makuu,
Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo.
K. Atalikumbuka agano lake milele.
Amewapa wamchao chakula;
Atalikumbuka agano lake milele.
Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake.
Kwa kuwapa urithi wa mataifa.
K. Atalikumbuka agano lake milele.
Amewapelekea watu wake ukombozi.
Ameamuru agano lake liwe la milele,
Jina lake ni takatifu la kuogopwa.
K. Atalikumbuka agano lake milele.
Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima,
Wote wafanyao hayo wana akili njema,
Sifa zake zakaa milele.
K. Atalikumbuka agano lake milele.
Shangilio la Injili
Mt. 4 : 4Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Aleluya.
Injili
Mk. 10:17-27Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu! Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu! Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu, Nao wakashangaa mno, wakimwambia, Ni nani, basi, awezaye kuokoka? Yesu akawakazia macho, akasema, Kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo; maanayoteyawezekana kwa Mungu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni