Sherehe ya Epifania
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Isa. 60:1-6Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 72:1-2, 7-8, 10-13Mataifa yote ya ulimwengu, watakusujudia, ee Bwana.
Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako.
Na mwana wa mfalme haki yako.
Atawaamua watu wako kwa haki,
Na watu wako walioonewa kwa hukumu.
K. Mataifa yote ya ulimwengu, watakusujudia, ee Bwana.
Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi,
Na wingi wa Amani hata mwezi utakapokoma
Na awe na enzi toka bahari hata bahari,
Toka mto hata miisho ya dunia.
K. Mataifa yote ya ulimwengu, watakusujudia, ee Bwana.
Wafalme wa Tarshisi na visiwa walete kodi,
Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.
Naam, wafalme wote na wamsujudie;
Na mataifa yote wamtumikie.
K. Mataifa yote ya ulimwengu, watakusujudia, ee Bwana.
Kwa maana atamwokoa mhitaji aliapo,
Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi
Atamhurumia aliye dhaifu na maskini,
Na nafsi za wahitaji ataziokoa.
K. Mataifa yote ya ulimwengu, watakusujudia, ee Bwana.
Somo la Pili
Efe. 3:2-3, 5-6Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho; ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Mt. 2:2Tuliona nyota yake mashariki, Nasi tumekuja kumsujudia.
Aleluya.
Injili
Mt. 2:1-12Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni