Kumbukumbu ya Wat. Yoakim Na Anna, wazazi wa Bikir
· Mwaka B
Somo la Kwanza
Yer. 2:1–3, 7–8, 12–13Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 36:5–10Kwako Bwana iko chemchemi ya uzima.
Ee Bwana, fadhili zako zafika hata mbinguni,
Uaminifu wako hata mawinguni.
Haki yako ni kama milimo ya Mungu,
Hukumu zako ni vilindi vikuu.
K. Kwako Bwana iko chemchemi ya uzima.
Ee Bwana, unawaokoa wanadamu na wanyama.
Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhila zako!
Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.
Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako,
Nawe utawanywesha mto wa furaha zako.
K. Kwako Bwana iko chemchemi ya uzima.
Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima,
Katika nuru yako tutaona nuru.
Uwadumishie wakujuao fadhili zako,
Na wanyofu wa moyo uaminifu wako.
K. Kwako Bwana iko chemchemi ya uzima.
Shangilio la Injili
Zab. 147:12, 15Msifu Bwana, ee Yerusalemu, huipeleka amri yake juu ya nchi.
Aleluya.
Injili
Mt. 13:10–17Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia. Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni