Alhamisi katika Oktava ya Pasaka
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Mdo 3:11-26Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 8:1, 4-8 au AleluyaWewe, Mungu, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni;
Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?
(K)Ee, Mungu, Bwana wetu; jinsi lilivyo tukufu jna lako duniani mwote
Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;
Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
(K)Ee, Mungu, Bwana wetu; jinsi lilivyo tukufu jna lako duniani mwote
Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni;
Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.
(K)Ee, Mungu, Bwana wetu; jinsi lilivyo tukufu jna lako duniani mwote
Injili
Lk 24:35-48Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Wakashituka, wakaogopa sana, wakidhani ya kwamba wanaona roho.
Akawaambia, Mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu?
Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo. Na baada ya kusema hayo aliwaonyesha mikono yake na miguu yake. Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula cho chote hapa? Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa. Akakitwaa, akala mbele yao. Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni