Jumatatu ya 23 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Kol. 1:24 – 2:3Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 62:5-6, 8Kwa Mungu wokovu wangu na utukufu wangu.
Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa kimya,
Tumaini langu hutoka kwake.
Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,
Ngome yangu, sitatikisika sana.
K. Kwa Mungu wokovu wangu na utukufu wangu.
Enyi watu, mtumainini siku zote,
Ifunueni mioyo yenu mbele zake;
Mungu ndiye kimbilio letu.
K. Kwa Mungu wokovu wangu na utukufu wangu.
Shangilio la Injili
Zab 19:8Amri ya Bwana ni safi,
huyatia macho nuru.
Aleluya.
Injili
Lk. 6:6-11Ndipo Yesu akawaambia, Nawauliza ninyi, Je! Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya; kuponya roho au kuangamiza? Akawakazia macho wote pande zote, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena. Wakajawa na uchungu, wakashauriana wao kwa wao wamtendeje Yesu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni