Kumbukumbu ya Mtakatifu Domniko
· Mwaka A · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Hes 12: 1-13Bwana akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje. Bwana akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama pale mlangoni pa Hema, aka- waita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.
Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, Bwana, nitajifunua kwake katika maono, nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; kwake nitanena mdomo kwa mdomo, maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?
Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake. Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya Hema; na tazarna, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazarna, yu mwenye ukoma.
Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu. nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanva dhambi. Nakusihi, asiwe kama mmoja aliyekufa, ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake. Musa akamlingana Bwana, akasema, Mpoze, Ee Mungu, nakusihi sana.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 51: 1-5, 10-11Ee Mungu uturehemu, kwa kuwa tumefanya dhambi.
Ee Mungu unirehemu, sawasawa na fadhili zako.
Kiasi cha wingi wa rehema zako,
uyafute makosa yangu.
K. Ee Mungu uturehemu, kwa kuwa tumefanya dhambi.
Unioshe kabisa na uovu wangu,
unitakase dhambi zangu.
Maana nimejua mimi makosa yangu,
na dhambi yangu i rnbcle yangu daima.
K. Ee Mungu uturehemu, kwa kuwa tumefanya dhambi.
Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo,
Na kuwa safi utoapo hukumu.
Tazarna, mimi naliumbwa katika hali ya uovu;
Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
K. Ee Mungu uturehemu, kwa kuwa tumefanya dhambi.
Ee Mungu, uniumbie moyo safi,
Uifanye upya roho iliyotuiia ndani yangu.
Usinitengc na uso wako,
Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.
K. Ee Mungu uturehemu, kwa kuwa tumefanya dhambi.
Shangilio la Injili
Zab 19: 8Amri ya Bwana ni safi, huyatia macho nuru.
Aleluya.
Injili
Mt. 14:22-36Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. Lakini alipouona upepo. akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? Nao walipopanda chomboni, upepo ulikoma. Nao waliokuwamo ndani ya chombo wakamsujudia, wakisema, Hakika wewe u Mwana wa Mungu.
Na walipokwisha kuvuka, walifika nchi ya Genesareti. Na watu wa mahali pale walipomtambua, walituma watu kwenda nchi zile zilizo kandokando, wakamletea wote waliokuwa hawawezi; nao wakamsihi waguse hata pindo la vazi lake tu; na wote waliogusa wakaponywa kabisa.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni