SIKUKUU YA KUNG’ARA BWANA WETU
· Mwaka A · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Dan 7: 9-10, 13-14Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu nave. Nave akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo haitapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 97 : 1-2, 5-6, 9Bwana ametamalaki, juu sana kuliko nchi yote.
K. Bwana ametamalaki, juu sana kuliko nchi yote.
Bwana ametamalaki, nchi na ishangilie,
Visiwa vingi na vifurahi.
Mawingu na giza vyamzunguka,
Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake. (K)
Milima iliyeyuka kama nta mbele za Bwana,
Mbele za Bwana wa dunia yote.
Mbingu zimetangaza haki yake,
Na watu wote wameuona utukufu wake. (K)
Maana Wewe, Bwana, ndiwe Uliye juu,
Juu sana kuliko nchi yote;
Umetukuka sana juu ya miungu yote. (K)
Somo la Pili
2 Pet. 1:16-19Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Mt 17: 5Huyu ni mwanangu, mpendwa wangu,
ninayependezwa naye, msikieni yeye.
Aleluya.
Injili
Mt 17: 1-9Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu ye yote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni