Jumanne ya 12 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mwa. 13 : 2, 5-18Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla Bwana hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya Bwana, kama nchi ya Misri hapo unapowenda Soari. Basi Lutu akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa mashariki; wakatengana wao kwa wao. Abramu akakaa katika nchi ya Kanaani, na Lutu akakaa katika miji ya lile Bonde; akajongeza hema yake mpaka Sodoma. Lakini watu wa Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya Bwana.
Bwana akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi; maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele. Na uzao wako nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi; hata mtu akiweza kuyahesabu mavumbi ya nchi, na uzao wako nao utahesabika. Ondoka, ukatembee katika nchi hii, katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo. Basi Abramu akajongeza hema yake akaja akakaa kwenye mialoni ya Mamre, nayo ni miti iliyoko Hebroni, akamjengea Bwana madhabahu huko.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 15:1-5Bwana ni nani atakayekaa katika hema yako?
Bwana ni nani atakayekaa katika hema yako?
Ni mtu aendaye kwa ukamilifu na kutcnda haki
asemaye kweli kwa moyo wake.
K. Bwana ni nani atakayekaa katika hema yako?
Asiyesingizia kwa ulimi wake,
Wala hakumtenda mwenziwe mabaya,
Wala hakumsengenya jirani yake.
Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa.
Bali huwaheshimu wamchao Bwana.
K. Bwana ni nani atakayekaa katika hema yako?
Hakutoa fedha yake apatc kula riba,
Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia.
Mtu atendaye mambo hayo
Hataondoshwa milele.
K. Bwana ni nani atakayekaa katika hema yako?
Shangilio la Injili
Zab. 119:105Neno lako ni taa ya miguu yangu,
na mwanga wa njia yangu.
Aleluya.
Injili
Mt. 7:6,12-1Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni