Jumatatu ya 12 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mwa. 12 : 1-9Basi Abramu akaenda, kama Bwana alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano aiipotoka Harani. Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia, na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani.
Abramu akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa More. Na Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo. Bwana akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu Bwana aliyemtokea. Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki; akamjengea Bwana madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana. Naye Abramu akasafiri, akazidi kwenda pandc za kusini.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 33 :12-13,18-20,22Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake.
Heri watu aliowachagua kuwa urithi wakc.
Toka mbinguni Bwana huchungulia,
Huwatazama wanadamu wote pia.
K. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake.
Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao,
Wazingojeao faadhili zakc.
Yeye huwaponya nafsi zao na mauti,
Na kuwahuisha wakati wa njaa.
K. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake.
Nafsi zetu zinamngoja Bwana;
Yeye ndiyc msaada wetu na ngao yetu.
Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi,
Kama vile tulivyokungoja Wewe.
K. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake.
Shangilio la Injili
Zab.l9:8Amri ya Bwana ni sali,
huyatia macho nuru.
Aleluya.
Injili
Mt. 7:1-5Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni