Jumamosi ya 3 ya Kwaresima
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Hos 5:15-6:6Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu. Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake. Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua Bwana; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujilia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi. Ee Efraimu, nikutendee nini? Ee Yuda, nikutendee nini? Kwa maana fadhili zenu ni kama wingu la asubuhi na kama umande utowekao mapema. Kwa sababu hiyo nimewakata-kata kwa vinywa vya manabii; nimewaua kwa maneno ya kinywa changu; na hukumu yangu itatokea kama mwanga. Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 51:1-2, 16-19Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.
Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu.
(K)Maana nataka fadhili wala si sadaka
Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa, Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa.
Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.
(K)Maana nataka fadhili wala si sadaka
Uitendee mema Sayuni kwa radhi yako, Uzijenge kuta za Yerusalemu.
Ndipo utakapopendezwa na dhabihu za haki, Na sadaka za kuteketezwa, na kafara.
(K)Maana nataka fadhili wala si sadaka
Injili
Lk 18:9-14Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni