Jumatatu ya 29 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Efe 2:1–10Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 100Ndiye aliyetuumba, na sisi tu watu wake.
Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote;
Mtumikieni Bwana kwa furaha;
Njoni mbele zake kwa kuimba.
K. Ndiye aliyetuumba, na sisi tu watu wake.
Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
K. Ndiye aliyetuumba, na sisi tu watu wake.
Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani mwake kwa kusifu;
Mshukuruni, lihimidini jina lake.
K. Ndiye aliyetuumba, na sisi tu watu wake.
Kwa kuwa Bwana ndiye mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi.
K. Ndiye aliyetuumba, na sisi tu watu wake.
Shangilio la Injili
Yn 8:12Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya.
Injili
Lk 12:13-21Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni