Jumanne ya 16 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mik 7:14–15, 18–20Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 85:1–7Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako.
Bwana, umeiridhia nchi yako,
Umewarejeza mateka wa Yakobo.
Umeusamehe uovu wa watu wako,
Umezisitiri hatia zao zote.
Umeiondoa ghadhabu yako yote,
Umerudi na kuuacha ukali wa hasira yako.
K. Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako.
Mungu wa wokovu wetu, uturudishe,
Uikomeshe hasira uliyo nayo juu yetu.
Je! Utatufanyia hasira hata milele?
Utadumisha ghadhabu kizazi hata kizazi.
K. Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako.
Je! Hutaki kurudi na kutuhuisha,
Watu wako wakufurahie?
Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako,
Utupe wokovu wako.
K. Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako.
Shangilio la Injili
2Kor 5:19Mungu alikuwa ndani ya Kristu, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake. Ametia ndani yetu neno la upatanisho.
Aleluya.
Injili
Mt 12:46–50Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (2)
Boniface Jelemia · 21 Julai 2026
Nimejifunza katika injili. Inatuambia tumpende mungu tumtumikie tumjue pia tutende matendo ya mpendezayo yeye aliye juu mbinguni
Sebastian Mavukilo · 21 Julai 2026
Bwana Yesu Asifiwe sana. Tumsifu Yesu Kristo. Leo maandiko yanatukumbusha upendo mkuu wa Mungu juu ya watu wake. Anatupenda kiasi cha kutodumisha hasira na gadhabu yake juu yetu; vyote huwepo kwa muda tu na baadae huviachilia. Aliamua hata kumtoa mwanae wa pekee ili kujipatanisha nasi. Lakini kuachilia huko huja baada ya sisi kuacha njia zetu za machukizo na kumwelekea yeye. Hivi ndio tutakuwa ndugu zake Bwana wetu Yesu Kristo, kama INJILI inavyoelekeza. SALA Eeh Mungu tunaomba utuumbie mioyo mipya iliyojaa hofu na utii wa NENO lako ili uweze kutuunganisha katika familia yako. Amina.