Jumamosi ya 15 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mik 2:1–5Awagawia waasi mashamba yetu. Kwa hiyo hutakuwa na mtu atakayeitupa Kamba kwa kura katika mkutano wa Bwana.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 10:1–4, 7–8, 14Usiwasahau wanyonge, Ee Bwana.
Ee Bwana, kwa nini wasimama mbali?
Kwa nini kujificha nyakati za shida?
Kwa kiburi chake asiye haki
Mnyonge anafuatiwa kwa ukali;
Na wanaswe kwa hila zizo hizo walizoziwaza.
K. Usiwasahau wanyonge, Ee Bwana.
Maana mdhalimu hujisifia tamaa ya nafsi yake,
Na mwenye choyo humkana Bwana na kumdharau.
Mdhalimu kwa kiburi cha uso wake
Asema, Hatapatiliza.
Jumla ya mawazo yake ni, Hakuna Mungu.
K. Usiwasahau wanyonge, Ee Bwana.
Kinywa chake kimejaa laana,
Na hila na dhuluma.
Chini ya ulimi wake kuna madhara na uovu,
Hukaa katika maoteo ya vijivi.
Mahali pa siri humwua asiye na hatia,
Macho yake humvizia mtu duni.
K. Usiwasahau wanyonge, Ee Bwana.
Umeona, maana unaangalia madhara na jeuri,
Uyatwae mkononi mwako.
Mtu duni hukuachia nafsi yake,
Maana umekuwa msaidizi wa yatima.
K. Usiwasahau wanyonge, Ee Bwana.
Shangilio la Injili
Yn 14:23Mtu akinipenda, atalishika neno langu, na Baba yangu atampenda, na sisi tutakuja kwake.
Aleluya.
Injili
Mt 12:14–21Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
JOHN UTENGA · 18 Julai 2026
Nashauri kama inawezekana tusaidiwe tafakari ya masomo husika ili itujenge zaidi.
alhaji japhary · 18 Julai 2026
Tumsifu Yesu Kristo! Rudi Sehemu ya Mwanzo shuka chini kabisa utaona TAFAKARI ya kila masomo inapatikana huko.