Pentekoste
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Mdo 2:1-11Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 104:1, 24, 29-31, 34Waipeleka roho yako, Ee Bwana, Nawe waufanya upya uso wa nchi.
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Wewe, Bwana, Mungu wangu,
Umejifanya mkuu sana;
Umejivika heshima na adhama.
Ee Bwana, jinsi yalivyo mengi matendo yako!
Kwa hekima umevifanya vyote pia.
Dunia imejaa mali zako.
K. Waipeleka roho yako, Ee Bwana, Nawe waufanya upya uso wa nchi.
Wewe wauficha uso wako,
Wao wanafadhaika;
Waiondoa pumzi yao, wanakufa,
Na kuyarudia mavumbi yao,
Waipeleka roho yako, wanaumbwa,
Nawe waufanya upya uso wa nchi.
K. Waipeleka roho yako, Ee Bwana, Nawe waufanya upya uso wa nchi.
Utukufu wa Bwana na udumu milele;
Bwana na ayafurahie matendo yake.
Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake;
Mimi nitamfurahia Bwana.
K. Waipeleka roho yako, Ee Bwana, Nawe waufanya upya uso wa nchi.
Somo la Pili
1Kor 12:3b-7, 12-13Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
ShangilioUje Roho Mtakatifu, uzienee nyoyo za waamini wako uwatie mapendo yako.
Aleluya
Injili
Yn 20:19-23Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (5)
LIVINUS MUKYANUZI · 24 Mei 2026
AMINA
Paul Chamtepa · 24 Mei 2026
Palipo roho yote yanawezekana
alhaji japhary · 24 Mei 2026
Sifa Kwako Eeh Kristo
Kamgisha Elipidius · 24 Mei 2026
Uje roho mtakatifu njoo kwenye familia yetu tujalie mapaji tuokoe zidi ya magonjwa yote yanayo tukabili.Tujalie baraka tele hapa duniani pia tunakuomba bikra maria mwombezi wa family utuombee
Timothy Sege Mwakisale · 24 Mei 2026
Sifa kwako eeh Kristu