Jumamosi ya 4 ya Mwaka
· Mwaka A
Somo la Kwanza
Ebr. 13:15 – 17, 20 – 21Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.
Basi, Mungu wa Amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu, awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake; naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amina.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 23Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
Bwana ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu.
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,
Kando ya maji ya utulivu huniongoza,
Hunihuisha nafsi yangu.
K. Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
Aliniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
Naam, nijapopita katika ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya,
Kwa maana Wewe upo pamoja nami.
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
K. Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
Waandaa meza mbele yangu
Machoni pa watesi wangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
Na kikombe changu kinafurika.
K. Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
Hakika wema na fadhili zitanifuata
Siku zote za maisha yangu;
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.
K. Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.
Shangilio la Injili
Zab. 119:105Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.
Aleluya.
Injili
Mk. 6:30-34Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni