JUMATANO YA 2 YA NOELI
· Mwaka A
Somo la Kwanza
1Yoh. 3:7-10Katika hili watoto wa Mungu ni Dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu yeyote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 98:1, 7-9Miisho yote ya dunia, imeuona Wokovu wa Mungu wetu.
Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Mkono wa kuume wake mwenyewe,
Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.
K. Miisho yote ya dunia, imeuona Wokovu wa Mungu wetu.
Bahari na ivume na vyote viijazavyo,
Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake.
Mito na ipige makofi,
Milima na iimbe pamoja kwa furaha,
Mbele za Bwana,
Kwa maana anakuja aihukumu nchi.
K. Miisho yote ya dunia, imeuona Wokovu wa Mungu wetu.
Atauhukumu ulimwengu kwa haki,
Na mataifa kwa adili.
K. Miisho yote ya dunia, imeuona Wokovu wa Mungu wetu.
Shangilio la Injili
Yn. 1:14,12Naye neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu.
Aleluya.
Injili
Yn. 1:35-42Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohane na kumfuata Yesu. Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo). Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohane; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni