Ijumaa ya 6 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mwa 11:1–9Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 33:10–15Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.
Bwana huyabatilisha mashauri ya mataifa,
Huyatangua makusudi ya watu.
Shauri la Bwana lasimama milele,
Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi.
K. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.
Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao,
Watu aliowachagua kuwa urithi wake.
Toka mbinguni Bwana huchungulia,
Huwatazama wanadamu wote pia.
K. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.
Toka mahali pake aketipo,
Huwaangalia wote wakaao duniani.
Yeye aiumbaye mioyo yao wote
Huzifikiri kazi zao zote.
K. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.
Shangilio la Injili
Zab 119:13Umwangazie mtumishi wako uso wako, na kunifundihsa amri zako.
Aleluya.
Injili
Mk 8:34–9:1Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni