Kumbukukumbu ya Mt. Fransisco Xavier Cabrini, Bikira,
· Mwaka B · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Tit. 3:1-7Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 23Bwana ndiye mchungaji wangu.
Bwana ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu.
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,
Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
Huniuisha nafsi yangu.
K. Bwana ndiye mchungaji wangu.
Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake,
Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya,
Kwa maana Wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
K. Bwana ndiye mchungaji wangu.
Waandaa meza mbele yangu,
Machoni pa watesi wangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
Na kikombe changu kinafurika.
K. Bwana ndiye mchungaji wangu.
Hakika wema na fadhili zitanifuata,
Siku zote za maisha yangu;
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.
K. Bwana ndiye mchungaji wangu.
Shangilio la Injili
Zab. 19:11-19Amri ya Bwana ni safi, huyatia macho nuru.
Aleluya.
Injili
Lk. 17:11-19Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu; akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria. Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu? Akamwambia, Inuka, enenda zako, Imani yako imekuokoa.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni