Sikukuu ya Kutabarukiwa Basilika la Laterani
· Mwaka B
Somo la Kwanza
Eze 47:1-2, 8-9, 12Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 46:1-2, 4-5, 7-8Vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye juu.
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,
Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi,
Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
K. Vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye juu.
Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu,
Patakatifu pa maskani zake Aliye juu.
Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa;
Mungu atausaidia asubuhi na mapema.
K. Vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye juu.
Bwana wa majeshi yu pamoja nasi,
Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
Njoni myatazame matendo ya Bwana,
Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.
K. Vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye juu.
Somo la Pili
1Kor 3:9-11, 16-17Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, nay a kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
2Nya 7:16Nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, asema Bwana, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele.
Aleluya.
Injili
Yn 2:13-22Basi Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya haya? Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, name katika siku t atu nitalisimamisha. Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu? Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake. Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
Alfredy Kilala · 9 Novemba 2024
Tumshukuru Mungu