Jumatano ya 22 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
1Kor 3:1–9Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. Basi yeye apandaye, nay eye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe. Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jingo la Mungu.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 33:12–15, 20–21Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake.
Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao,
Watu aliowachagua kuwa urithi wake.
Toka mbinguni Bwana huchungulia,
Huwatazama wanadamu wote pia.
K. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake.
Toka mahali pake aketipo
Huwaangalia wote wakaao duniani.
Yeye aiumbaye mioyo yao wote
Huzifikiri kazi zao zote.
K. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake.
Nafsi zetu zinamngoja Bwana;
Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
Maana mioyo yenu itamfurahia,
Kwa kuwa tumelitumainia jina lake takatifu.
K. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake.
Shangilio la Injili
Yak 1:21Pokeeni kwa upole neno la Mungu lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.
Aleluya.
Injili
Lk 4:38–44Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni