Kumbukumbu ya Mt. Gregori Mkuu, Papa na Daktari wa Kanisa
· Mwaka B · Juma la 2 la Zaburi
Somo la Kwanza
1Kor 2:10–16Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni kuyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. Maana, ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 145:8–14Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote.
Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma,
Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,
Bwana ni mwema kwa watu wote,
Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.
K. Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote.
Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru,
Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
Wataunena utukufu wa ufalme wako,
Na kuuhadithia uweza wako.
Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
K. Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote.
Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.
Bwana huwategemeza wote waangukao,
Huwainua wote walioinama chini.
K. Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote.
Shangilio la Injili
Ebr 4:12Neno la Mungu li hai tena li na nguvu, li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Aleluya.
Injili
Lk 4:31–37Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni