Alhamisi ya 20 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Eze 36:23–28Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 51:10: -13, 16–17Nitawanyunyizia maji safi, Nanyi mtakuwa safi, nitawatakaseni na uchafu wenu wote.
Ee Mungu, uniumbie moyo safi,
Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu.
Usinitenge na uso wako,
Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.
K. Nitawanyunyizia maji safi, Nanyi mtakuwa safi, nitawatakaseni na uchafu wenu wote.
Unirudishie furaha ya wokovu wako;
Unitegemeze kwa roho ya wepesi.
Nitawafundisha wakosaji njia zako,
Na wenye dhambi watarejea kwako.
K. Nitawanyunyizia maji safi, Nanyi mtakuwa safi, nitawatakaseni na uchafu wenu wote.
Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa,
Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa.
Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika;
Moyo uliovunjika na kupondeka,
Ee Mungu, hutaudharau.
K. Nitawanyunyizia maji safi, Nanyi mtakuwa safi, nitawatakaseni na uchafu wenu wote.
Shangilio la Injili
Zab 19:8Amri ya Bwana ni safi, huyatia macho nuru.
Aleluya.
Injili
Mt 22:1–14Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni