Sikukuu ya Mt. Yakobo, Mtume
· Mwaka B
Somo la Kwanza
2Kor 4:7-15Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 126Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha
Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni,
Tulikuwa kama waotao ndoto.
Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko,
Na ulimi wetu kelele za furaha.
K. Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha
Ndipo waliposema katika mataifa,
Bwana amewatendea mambo makuu.
Bwana alitutendea mambo makuu,
Tulikuwa tukifurahi.
K. Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha
Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa,
Kama vijito vya Kusini.
Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.
K. Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha
Ingawa mtu anakwenda zake akilia,
Azichukuapo mbegu za kupanda.
Hakika atarudi kwa kelele za furaha,
Aichukuapo miganda yake.
K. Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha
Shangilio la Injili
Yn 15:16Ni mimi niliyewachagua ninyi nikawaweka mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kukaa, asema Bwana
Aleluya
Injili
Mt 20:20-28Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni