Jumatano ya 16 ya Mwaka C
· Mwaka B · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yer 1:1, 4-10Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 71:1-6, 15, 17Kinywa changu kitasimulia haki na wokovu wako.
Nimekukimbilia Wewe, Bwana, Nisiaibike milele.
Kwa haki yako uniponye, uniopoe, Unitegee sikio lako, uniokoe.
K. Kinywa changu kitasimulia haki na wokovu wako.
Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu, Nitakakokwenda sikuzote. Umeamuru niokolewe, Ndiwe genge langu na ngome yangu.
Ee Mungu wangu, uniopoe mkononi mwa mkorofi, Katika mkono wake mwovu, mdhalimu,
K. Kinywa changu kitasimulia haki na wokovu wako.
Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU, Tumaini langu tokea ujana wangu.
Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa, Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, Ninakusifu Wewe daima.
K. Kinywa changu kitasimulia haki na wokovu wako.
Kinywa changu kitasimulia haki na wokovu wako Mchana kutwa; maana sijui hesabu yake.
Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu; Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata leo.
K. Kinywa changu kitasimulia haki na wokovu wako.
Shangilio la Injili
.Neno la Mungu ni mbegu, na Kristu ndiye mpanzi, wote watakaokuja kwake wataishi milele.
Aleluya
Injili
Mt 13:1-9Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni