Jumanne ya 15 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Isa 7:1–9Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 48:1–7Mji wa mungu wetu ataufanya imara hata milele.
Bwana ndiye aliye mkuu,
Na mwenye kusifiwa sana.
Katika mji wa Mungu wetu,
Katika mlima wake mtakatifu.
Kuinuka kwake ni mzuri sana,
Ni furaha ya dunia yote.
K. Mji wa mungu wetu ataufanya imara hata milele.
Mlima Sayuni pande za kaskazini,
Mji wa Mfalme mkuu.
Mungu katika majumba yake
Amejijulisha kuwa ngome.
K. Mji wa mungu wetu ataufanya imara hata milele.
Maana, tazama, wafalme walikusanyika;
Walipita wote pamoja.
Waliona, mara wakashangaa;
Wakafadhaika na kukimbia.
K. Mji wa mungu wetu ataufanya imara hata milele.
Papo hapo tetemeko liliwashika,
Utungu kama wa mwanamke azaaye.
Kwa upepo wa mashariki
Wavunja jahazi za Tarshishi.
K. Mji wa mungu wetu ataufanya imara hata milele.
Shangilio la Injili
Zab 119:34Unifahamishe name nitaishika sharia yako, nitaitii kwa moyo wangu wote.
Aleluya.
Injili
Mt 11:20–24Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni