Sherehe ya Utatu Mtakatifu
· Mwaka B
Somo la Kwanza
Kum 4 :32-34, 39-40Kwa hiyo ujue, leo hivi, ukaweke moyoni mwako, ya kuwa Bwana ndiye Mungu katika mbingu juu, na katika nchi chini; hapana mwingine. Basi, zishike sheria zake, na amri zake, ninazokuamuru leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako, na siku zako ziwe nyingi katika nchi ile akupayo Bwana, Mungu wako, milele.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 33 :4-6, 9, 18-20, 22Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.
Kwa kuwa neno la Bwana ni adili,
Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.
Bwana huzipenda haki na hukumu,
Nchi imejaa fadhili za Bwana.
K. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.
Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika.
Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake.
Maana Yeye alisema, ikawa;
Na Yeye aliamuru, ikasimama.
K. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.
Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao,
Wazingojeao fadhili zake.
Yeye huwaponya nafsi zao na mauti,
Na kuwahuisha wakati wa njaa.
K. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.
Nafsi zetu zinamngoja Bwana,
Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi,
Kama vile tulivyokungoja Wewe.
K. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.
Somo la Pili
Rum 8 :14-17Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Ufu 1:8Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, Mungu ambaye yupo, aliyekuwako, na atakayekuja.
Aleluya.
Injili
Mt 28: 16-20Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
hyacinth mapunda · 26 Mei 2024
Amina