Jumamosi ya 7 ya mwaka
· Mwaka B · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yak 5:13–20Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza; jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 141: 1–3, 8Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba.
Ee Bwana, nimekuita, unijie hima,
Uisikie sauti yangu nikuitapo.
Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba,
Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.
K. Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba.
Ee Bwana, uweke mlinzi kinywani pangu,
Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.
Macho yangu yanakuelekea Wewe, Mungu Bwana,
Nimekukimbilia Wewe, usiniache nafsi yangu.
K. Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba.
Shangilio la Injili
Yn 17:17Neno lako ndiyo kweli, ee Bwana, ututakase kwa ile kweli.
Aleluya.
Injili
Mk 10:13–16Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (1)
Martin Muteti · 25 Mei 2024
Amina