Jumatatu ya 25 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Ezr 1:1-6Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 126Bwana alitutendea mambo makuu.
Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni,
Tulikuwa kama waotao ndoto.
Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko,
Na ulimi wetu kelele za furaha.
Ndipo waliposema katika mataifa,
“Bwana amewatendea mambo makuu”.
K. Bwana alitutendea mambo makuu.
Bwana alitutendea mambo makuu,
Tulikuwa tukifurahi.
Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa,
Kama vijito vya Kusini.
K. Bwana alitutendea mambo makuu.
Wapandao kwa machozi
Watavuna kwa kelele za furaha.
Ingawa mtu anakwenda zake akilia,
Azichukuapo mbegu za kupanda,
Hakika atarudi kwa kelele za furaha,
Aichukuapo miganda yake.
K. Bwana alitutendea mambo makuu.
Shangilio la Injili
Yak 1:18Kwa kupenda kwake mwenyewe, Baba alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake.
Aleluya.
Injili
Lk 8:16–18Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni