Ijumaa ya 24 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
1Tim 6:2-12Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, Imani, upendo, saburi, upole. Piga vita vile vizuri vya Imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 49:5-9, 16-19Heri walio maskini war oho, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Kwa nini niogope siku za uovu,
Ubaya ukinizunguka miguuni pangu?
Wa hao wanaozitumainia mali zao,
Na kujisifia wingi wa utajiri wao.
K. Heri walio maskini war oho, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake,
Wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake,
Maana fidia ya nafsi zao ina gharama,
Wala hana budi kuiacha hata milele.
Ili ishi sikuzote asilione kaburi.
K. Heri walio maskini war oho, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Usiogope mtu atakapopata utajiri
Na fahari ya nyumba yake itakapozidi.
Maana atakapokufa hatachukua chochote;
Utukufu wake hautashuka ukimfuata.
K. Heri walio maskini war oho, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Ajapojibariki nafsi yake alipokuwa hai,
Na watu watakusifu ukijitendea mema,
Atakwenda kwenye kizazi cha baba zake,
Hawataona nuru hata milele.
K. Heri walio maskini war oho, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Shangilio la Injili
Zab 19:8Amri ya Bwana ni safi, huyatia macho nuru.
Aleluya.
Injili
Lk 8:1–3Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni