Jumatatu ya 20 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Amu 2: 11-19Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 106: 34-37, 39-40, 43-44Ee Bwana, unikumbuke mimi, kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako.
Hawakuwaharibu watu wa nchi
Kama Bwana alivyowaambia;
Bali walijkhanganya na mataifa,
Wakajifunza matendo yao.
K. Ee Bwana, unikumbuke mimi, kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako.
Wakazitumikia sanamu zao,
Nazo zikawa mtego kwao.
Naam. walitoa wana wao na binti zao
Kuwa dhabihu kwa mashetani.
K. Ee Bwana, unikumbuke mimi, kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako.
Ndivyo walivyotiwa uchafu kwa kazi zao,
Wakafanya uasherati kwa matendo yao.
Hasira ya Bwana ikawaka juu ya watu wake,
Akauchukia urithi wake.
K. Ee Bwana, unikumbuke mimi, kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako.
Mara nyingi aliwaponya,
Bali walikuwa wakimwasi kwa mashauri yao,
Wakadhilika katika uovu wao.
Lakini aliyaangalia mateso yao,
Aliposikia kilio chao.
K. Ee Bwana, unikumbuke mimi, kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako.
Shangilio la Injili
1 Thes 2:13Lipokeeni neno la Mungu, siyo kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu.
Aleluya
Injili
Mt 19:16-22Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni