Jumatatu ya 16 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Kut 14:5-18Wakamwambia Musa, Je! kwa sababu hapakuwa na makaburi katika Misri umetutoa huko ili tufe jangwani? Mbona umetutendea haya, kututoa katika nchi ya Misri? Neno hili silo tulilokuambia huko Misri, tukisema, Tuache tuwatumikie Wamisri? Maana ni afadhali kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani. Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
Bwana akamwambia Musa, Mbona unanililia mimi? Waambie wana wa Israeli waendelee mbele. Nawe inua fimbo yako, ukanyoshe mkono wako juu ya bahari, na kuigawanya; nao wana wa Israeli watapita kati ya bahari katika nchi kavu. Nami, tazama, nitaifanya mioyo ya Wamisri kuwa migumu, nao wataingia na kuwafuatia, nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote, kwa magari yake na kwa wapanda farasi wake. Na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapokwisha kujipatia utukufu kwa Farao, na magari yake, na farasi zake.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Kut 15:1-6Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana.
Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana;
Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.
Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu;
Naye amekuwa wokovu wangu.
Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu;
Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.
K. Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana.
Bwana ni mtu wa vita,
Bwana ndilo jina lake.
Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini,
Maakida yake wateule wamezama katika bahari ya Shamu.
K. Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana.
Vilindi vimewafunikiza,
Walizama vilindini kama jiwe.
Bwana, mkono wako wa kuume
umepata fahari ya uwezo,
Bwana, mkono wako wa kuume wawasetaseta adui.
K. Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana.
Shangilio la Injili
Yn 15:15Bwana anasema: Siwaiti tena watumwa,
lakini ninyi nimewaita rafiki,
kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.
Aleluya.
Injili
Mt 12:38-42Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni