Dominika ya 16 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Hek. 12 :13.16-19Pamoja na hayo, uliwafundisha watu wako kwa matendo yako ya namna hiyo ya kwamba imempasa mwenye haki kuwa mpenda wanadamu; tena ukawatilia wanao tumaini jema, kwa sababu, endapo watu wametenda dhambi, unawajalia toba.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 86:5-6, 9-10, 15-16Kwa maana Wewe, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe.
Wewe, Bwana, U mwema,
Umekuwa tayari kusamehe.
Na mwingi wa fadhili,
Kwa watu wote wakuitao.
Ee Bwana, uyasikie maombi yangu;
Uisikilize sauti ya dua zangu.
K. Kwa maana Wewe, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe.
Mataifa yote uliowafanya watakuja;
Watakusujudia Wewe, Bwana.
Watalitukuza jina lako;
Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu.
Wewe ndiwe mfanya miujiza,
Ndiwe Mungu peke yako.
K. Kwa maana Wewe, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe.
Lakini Wewe, Bwana,
U Mungu wa rehema na neema.
Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli.
Unielekee na kunifadhili mimi.
K. Kwa maana Wewe, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe.
Somo la Pili
Rum 8 : 26-27Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Yn. 17:17Neno lako ndiyo kweli,
Ee Bwana, Ututakase sisi kwa ile kweli.
Aleluya.
Injili
Mt. 13:24-43Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake; nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake.
Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke. akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia. Hayo yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno; ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu awali.
Kisha Yesu akawaaga makutano, akaingia nyumbani; wanafunzi wake wakamwendea, wakasema, Tufafanulie mfano wa magugu ya kondeni. Akajibu, akasema, Azipandaye zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu; lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu; yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wa wavunao ni malaika. Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia. Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake; nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. Ndipo wenye haki watakapong’aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio, na asikie.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni