Jumatano ya 12 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 4 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mwa 15:1-12, 17-18Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 105:1-4,6-9Bwana analikumbuka agano lake milele.
Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake,
Wajulisheni watu matendo yake,
Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi,
Zitafakarini ajabu zake zote.
K. Bwana analikumbuka agano lake milele.
Jisifuni kwa jina lake takatifu,
Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.
Mtakeni Bwana na nguvu zake,
Utafuteni uso wake sikuzote.
K. Bwana analikumbuka agano lake milele.
Enyi wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake;
Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
Yeye, Bwana, ndiye Mungu wetu;
Duniani mwote mna hukumu zake.
K. Bwana analikumbuka agano lake milele.
Analikumbuka agano lake milele;
Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
Agano alilofanya na Ibrahimu,
uapo wake kwa Isaka.
K. Bwana analikumbuka agano lake milele.
Shangilio la Injili
Zab 147:12, 15Msifu Bwana, ee Yerusalemu, huipeleka amri yake juu ya nchi.
Aleluya.
Injili
Mt 7:15-20Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni