Alhamisi ya 11 ya Mwaka
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
2 Kor. 11:1 - 11Je! Nalifanya dhambi kwa kunyenyekea ili ninyi mtukuzwe, kwa sababu naliwahubiri Injili ya Mungu bila ujira? Naliwanyang’anya makanisa mengine mali yao, nikitwaa posho langu ili niwahudumie ninyi. Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote nalijilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena nitajilinda. Kama vile vile kweli ya Kristo ilivyo ndani yangu, hakuna mtu atakayenifumba kinywa katika kujisifu huku, katika mipaka ya Akaya. Kwa nini? Je! Ni kwa sababu siwapendi ninyi? Mungu anajua.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 111: 1-4, 7-8Matendo yako Bwana ni kweli na hukumu.
Aleluya.
Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote,
Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
K. Matendo yako Bwana ni kweli na hukumu.
Matendo ya Bwana ni makuu,
Na haki yake yakaa milele.
Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu;
Bwana ni mwenye fadhili na rehema.
K. Matendo yako Bwana ni kweli na hukumu.
Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu,
Maagizo yake yote ni amini,
Yamethibitika milele na milele,
Yamefanywa katika kweli na adili.
K. Matendo yako Bwana ni kweli na hukumu.
Shangilio la Injili
1The. 2:13Lipokeeni neno la Mungu, siyo kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu.
Aleluya.
Injili
Mt. 6:7-15Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliyembinguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu.
Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni