Jumanne ya 29 ya Mwaka
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Efe. 2:12 – 22Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe na jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jingo lote linaungamanishwa vema na kuku ahata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 85:9 – 14Bwana anawaambia watu wake amani.
Nisikie atakavyosema Bwana,
Maana atawaambia watu wake amani.
Hakika wokovu wake u karibu na wamchao,
Utukufu ukae katika nchi yetu.
K. Bwana anawaambia watu wake amani.
Fadhili na kweli zimekutana,
Haki na amani zimebusiana.
Kweli imechipuka katika nchi,
Haki imechungulia kutoka mbinguni.
K. Bwana anawaambia watu wake amani.
Bwana atatoa kilicho chema,
Na nchi yetu itatoa mazao yake.
Haki itakwenda mbele zake,
Nayo itazifanya hatua zake kuwa njia.
K. Bwana anawaambia watu wake amani.
Shangilio la Injili
Yn. 10:27Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.
Injili
Lk. 12:35-38Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni