Dominika ya 5 ya Pasaka
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Mdo 6:1-7Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 33:1-2, 4-5, 1-19Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi, Kama vile tulivyokungoja Wewe.
Mpigieni Bwana vigelcgele, enyi wenye haki,
Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
Mshukuruni Bwana kwa kinubi,
Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.
K. Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi, Kama vile tulivyokungoja Wewe.
Kwa kuwa neno la Bwana lina adili,
Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.
Huzipenda haki na hukumu,
Nchi imejaa fadhili za Bwana.
K. Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi, Kama vile tulivyokungoja Wewe.
Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao,
Wazingojeao fadhili zake.
Yeye huwaponya nafsi zao na mauti,
Na kuwahuisha wakati wa njaa.
K. Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi, Kama vile tulivyokungoja Wewe.
Somo la Pili
1Pet 2:4-9Na kila amwaminiye hatatahayarika. Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni. Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha. Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo.
Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Shangilio la Injili
Yn 14:6Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Aleluya.
Injili
Yn 14:1-12Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni