Jumanne ya 3 ya Majilio
· Mwaka A · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Sef 3:1-2, 9-13Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 34:1-2, 5-6, 16-17, 18, 22Maskini aliita, Bwana akasikia
Nitamhimidi Bwana kila wakati,
Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
Katika Bwana nafsi yangu itajisifu,
Wanyenyekevu wasikie wakafurahi.
K. Maskini aliita, Bwana akasikia
Wakamwelekea macho wakatiwa nuru,
Wala nyuso zao hazitaona haya.
Maskini huyu aliita, Bwana akasikia,
Akamwokoa na taabu zake zote.
K. Maskini aliita, Bwana akasikia
Uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya,
Aliondoe kumbukumbu lao duniani.
Walilia, naye Bwana akasikia,
Akawaponya na taabu zao zote.
K. Maskini aliita, Bwana akasikia
Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo,
Na waliopondeka roho huwaokoa.
Bwana huzikomboa nafsi za watumishi wake,
Wala hawatahukumiwa wote wamkimbiliao.
K. Maskini aliita, Bwana akasikia
Shangilio la Injili
ShangilioUje, Bwana, wala usikawie; Uzisamehe dhambi za taifa lako.
Aleluya.
Injili
Mt 21:28-32Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni