Jumanne ya 1 ya Majilio
· Mwaka A · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Isa 11:1-10Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kimono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng’ombe. Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira. Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari.
Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzika patakuwa na utukufu.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 72:1-2, 7-8, 12-13, 17Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi na wingi wa amani kwa milele.
Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako,
Na mwana wa mfalme haki yako
Atawaamua watu wako kwa haki,
Na watu wako walioonewa kwa hukumu.
K. Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi na wingi wa amani kwa milele.
Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi,
Na wingi wa amani hata mwezi utakapokoma.
Na awe na enzi toka bahari hata bahari,
Toka mto hata miisho ya dunia.
K. Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi na wingi wa amani kwa milele.
Kwa maana atamwokoa mhitaji aliapo,
Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi,
Atamhurumia aliye dhaifu na maskini,
Na nafsi za wahitaji ataziokoa.
K. Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi na wingi wa amani kwa milele.
Jina lake na lidumu milele,
Pindi ling’aapo jua jina lake liwe na wazao;
Mataifa yote na wajibariki katika yeye,
Na kumwita heri.
K. Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi na wingi wa amani kwa milele.
Shangilio la Injili
ShangilioTazama Bwana wetu atakuja na nguvu, na atayaangaza macho ya watumishi wake.
Aleluya.
Injili
Lk 10:21-24Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni