Jumatano ya 26 ya Mwaka
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Ayu. 9:1 – 12, 14 – 16Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab. 88:9 – 14Maombi yangu yafike mbele zako, Ee Bwana.
Bwana, nimekuita kila siku,
Nimekunyoshea Wewe mikono yangu.
Wafu je! Utawafanyia miujiza?
Au waliofariki watasimama na kukuhimidi?
K. Maombi yangu yafike mbele zako, Ee Bwana.
Fadhili zako zitasimuliwa kaburini?
Au uaminifu wako katika uharibufu?
Miujiza yako itajulikana gizani?
Au haki yako katika nchi ya usahaulifu?
K. Maombi yangu yafike mbele zako, Ee Bwana.
Lakini mimi nimekulilia Wewe, Bwana,
Na asubuhi maombi yangu yatakuwasilia.
Bwana, kwa nini kuitupa nafsi yangu,
Na kunificha uso wako?
K. Maombi yangu yafike mbele zako, Ee Bwana.
Shangilio la Injili
Mt. 4:4Mtu hataishi kwa mkate tu,
ila kwa kila neno litokalo
katika kinywa cha Mungu.
Aleluya.
Injili
Lk. 9:57-62Akamwambia mwingine, Nifuate. Akasema, Bwana, nipe ruhusu kwanza niende nikamzike baba yangu. Akamwambia, Waache wafu wawazike wafu; bali wewe enenda ukautangaze ufalme wa Mungu.
Mtu mwingine pia akamwambia, Bwana, nitakufuata; lakini, nipe ruhusu kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu. Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni