Jumamosi ya 29 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 1 la Zaburi
Somo la Kwanza
Efe 4:7–16Tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike kweli katika upendo na kuku ahata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.
Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 122:1–5Nalifurahi waliponiambia, na twende nyumbani kwa Bwana.
Nalifurahi waliponiambia,
Na twende nyumbani kwa Bwana.
Miguu yetu imesimama
Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu.
K. Nalifurahi waliponiambia, na twende nyumbani kwa Bwana.
Ee Yerusalmeu uliyejengwa
Kama mji ulioshikamana,
Huko ndiko waliopanda kabila,
Kabila za Bwana.
K. Nalifurahi waliponiambia, na twende nyumbani kwa Bwana.
Ushuhuda kwa Israeli,
Walishukuru jina la Bwana.
Maana huko viliwekwa viti vya hukumu,
Viti vya enzi vya mbari ya Daudi.
K. Nalifurahi waliponiambia, na twende nyumbani kwa Bwana.
Shangilio la Injili
2Tim 1:10Mwokozi wetu Yesu Kristo alibatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika kwa Injili.
Aleluya.
Injili
Lk 13:1-9Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafua matunda juu yake, asipate. Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu? Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni