Jumamosi ya 25 ya Mwaka
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Mh 11:9 - 12:8Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 90:3-6, 12-14, 17Wewe Bwana, umekuwa makao yetu, kikazi baada ya kizazi.
Wamrudisha mtu mavumbini, usemapo,
Rudini, enyi wanadamu.
Maana miaka elfu machoni pako
Ni kama siku ya jana ikiisha kupita,
Na kama kesha la usiku.
K. Wewe Bwana, umekuwa makao yetu, kikazi baada ya kizazi.
Wawagharikisha, huwa kama usingizi,
Asubuhi huwa kama majani yameayo.
Asubuhi yachipuka na kumea,
Jioni yakatika na kukauka.
K. Wewe Bwana, umekuwa makao yetu, kikazi baada ya kizazi.
Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu,
Tujipatie moyo wa hekima.
Ee Bwana urudi, hata lini?
Uwahurumie watumishi wako.
K. Wewe Bwana, umekuwa makao yetu, kikazi baada ya kizazi.
Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako,
Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.
Na uzuri wa Bwana, Mungu wetu, uwe juu yetu,
Na kazi ya mikono yetu utufanyie thabiti,
Naam, kazi ya mikono yetu uithibitishe.
K. Wewe Bwana, umekuwa makao yetu, kikazi baada ya kizazi.
Shangilio la Injili
2 Tim 1:10Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili;
Aleluya
Injili
Lk 9:43-45Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni