Alhamis ya 25 ya Mwaka
· Mwaka C
Somo la Kwanza
Mhu 1:2-11Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 90:3-6, 12-14, 17Wamrudisha mtu mavumbini, usemapo, Rudini, enyi wanadamu.
Maana miaka elfu machoni pako Ni kama siku ya jana ikiisha kupita, Na kama kesha la usiku.
(K)Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, kizazi baada ya kizazi
Wawagharikisha, huwa kama usingizi, Asubuhi huwa kama majani yameayo.
Asubuhi yachipuka na kumea, Jioni yakatika na kukauka.
(K)Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, kizazi baada ya kizazi
Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima.
Ee Bwana urudi, hata lini? Uwahurumie watumishi wako.
(K)Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, kizazi baada ya kizazi
Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako, Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.
Na kazi ya mikono yetu utufanyie thabiti, Naam, kazi ya mikono yetu uithibitishe.
(K)Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, kizazi baada ya kizazi
Shangilio la Injili
Zab. 27:11Ee Bwana, unifundihse njia yako,
na kuniongoza katika njia iliyonyoka.
Aleluya.
Injili
Lk 9:7-9Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni