Jumatatu ya 7 ya Mwaka
· Mwaka C · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
Yak 3:13-18Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 19:7-10Maagizo ya Bwana, huufurahisha moyo.
Sharia ya Bwana ni kamilifu,
Huiburudisha nafsi.
Ushuhuda wa Bwana ni amini,
Humtia mjinga hekima.
K. Maagizo ya Bwana, huufurahisha moyo.
Maagizo ya Bwana ni ya adili,
Huururahisha moyo.
Amri ya Bwana ni safi,
Huyatia macho nuru.
K. Maagizo ya Bwana, huufurahisha moyo.
Kicho cha Bwana ni kitakatifu,
Kinadumu milele.
Hukumu za Bwana ni kweli,
Zina haki kabisa.
K. Maagizo ya Bwana, huufurahisha moyo.
Ni za kutamanika kuliko dhahabu,
Kuliko wingi wa dhahabu safi.
Nazo ni tamu kuliko asali,
Kuliko sega la asali.
K. Maagizo ya Bwana, huufurahisha moyo.
Shangilio la Injili
Yak 1:21Pokeeni kwa upole neno la Mungu lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.
Aleluya.
Injili
Mk 9:14-29Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini; akagaagaa. Akitokwa na povu. Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, tangu utoto. Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwamngamize; lakini ukiweza neno lolote, utuhurumie, na kutusaidia. Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu. Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena. Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa. Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua; naye akasimama.
Hata alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa? Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lolote, isipokuwa kwa kuomba.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni