Jumamosi ya 23 ya Mwaka
· Mwaka B · Juma la 3 la Zaburi
Somo la Kwanza
1 Tim 1:15-17Neno la Bwana. — Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa Katikati
Zab 113:1-7Jina la Bwana lihimidiwe tangu leo na hata milele.
Aleluya.
Enyi watumishi wa Bwana, sifuni,
Lisifuni jina la Bwana,
Jina la Bwana lihimidiwe
Tangu leo na hata milele.
K. Jina la Bwana lihimidiwe tangu leo na hata milele.
Toka maawio ya jua hata machweo yake
Jina la Bwana husifiwa.
Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote,
Na utukufu wake ni juu ya mbingu.
K. Jina la Bwana lihimidiwe tangu leo na hata milele.
Ni nani aliye mfano wa Bwana,
Mungu wetu aketiye juu;
Anyenyekeaye kutazama,
Mbinguni na duniani?
Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Na kumpandisha maskini kutoka jaani.
K. Jina la Bwana lihimidiwe tangu leo na hata milele.
Shangilio la Injili
Lk 8:15Wanabarikiwa wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao, hulisikia neno la Mungu na kulishika.
Aleluya.
Injili
Lk 6:43 – 49Na kwa nini mnaniita, Bwana, walakini hamtendi nisemayo?
Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake. Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri. Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba yakawa makubwa.
Injili ya Bwana. — Sifa kwako, Ee Kristo.
Maoni (0)
Bado hakuna maoni. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.
Ingia utoe maoni